Umuhimu wa GPT Vyuo Vikuu Tanzania na Mapungufu Yake – Na Wazo la DIAR

Mwaka huu 2024, Tanzania inashuhudia mabadiliko makubwa katika elimu ya juu. ChatGPT, teknolojia ya Artificial Intelligence (AI) kutoka OpenAI, imeingia kwa kasi katika vyuo vikuu nchini. Kwa wanafunzi na walimu wengi, hii ni kama muujiza. Wanafunzi wanatumia GPT kutatua maswali magumu ya assignment, kuelewa dhana ngumu za somo, kuandika essays, na hata kufanya revision haraka. Walimu wanafurahia kuona wanafunzi wakitafuta maarifa zaidi nje ya darasa, na baadhi yao wanatumia GPT kuandaa mifano ya maswali au maelezo ya ziada.

Kwa ufupi, uwepo wa GPT umeleta furaha kubwa. Wanafunzi wanahisi wana “mwalimu wa kibinafsi” anayepatikana saa 24, na walimu wanaona teknolojia inasaidia kupunguza mzigo wa kuulizwa maswali yale yale mara nyingi. Lakini, kama teknolojia yoyote mpya, GPT ina mapungufu makubwa – hasa katika mazingira ya elimu ya Tanzania.

Mapungufu Makubwa ya GPT katika Elimu

Kwanza, GPT hajibu maswali kulingana na yale ambayo mwalimu amefundisha darasani. Anajibu kulingana na uelewa wake mwenyewe, ambao umejengwa kutokana na data nyingi sana kutoka mtandaoni na vitabu vya kimataifa. Hii ina maana kwamba jibu lake linaweza kuwa sahihi kwa mtazamo wa kimataifa, lakini lisiendane kabisa na mtaala, mifano, au msisitizo aliyotumia mwalimu wako. Mfano: mwalimu anaweza kufundisha dhana kwa kutumia mifano ya Tanzania au suala la ndani, lakini GPT anatoa mifano ya Marekani au Ulaya. Matokeo yake, mwanafunzi anaweza kujibu mtihani kwa njia isiyolingana na matarajio ya mwalimu.

Pili, ni rahisi sana kwa mwalimu kugundua majibu yaliyotoka kwa GPT. Mtindo wa lugha ya GPT unafanana sana – sentensi ndefu, muundo wa kawaida, na maneno yanayorudiwa. Walimu wengi sasa wanajua “sauti” ya GPT. Zaidi ya hayo, majibu ya GPT mara nyingi yana mapungufu yanayofanana: yanakosa muktadha wa ndani (context ya Tanzania), yanaweza kutoa taarifa za zamani, au hata “hallucinate” (kutoa taarifa za uongo zinazoonekana kuwa sahihi). Kwa wanafunzi, hii inaweza kusababisha kupoteza alama ikiwa wataandika majibu bila kuyachambua.

Tatu, GPT haielewi “notes” za mwanafunzi binafsi. Anajibu kwa ujumla, si kwa msingi wa maelezo uliyoandika darasani au yale uliyofundishwa na mwalimu wako. Hii inafanya iwe ngumu kwa mwanafunzi kupata jibu linalolingana kabisa na kile anachohitaji kwa mtihani au assignment yake.

Haya ni mapungufu yanayofanya GPT isiwe suluhisho kamili kwa elimu ya juu Tanzania, hasa katika vyuo ambapo mtaala na mbinu za ufundishaji zina tofauti na data ya kimataifa.

Wazo la DIAR – Suluhisho Linalotegemea Notes Zako

Hapa ndipo wazo la DIAR linapoingia. DIAR ni kifupi cha TADA Interpretation Analysis Response – jukwaa (mtandao) ambalo bado ni wazo, lakini linalokusudiwa kujengwa ili kutatua haswa mapungufu haya ya GPT katika mazingira ya elimu.

DIAR itakuwa tofauti kabisa:

  • Itachakata notes za wanafunzi. Mwanfunzi atapakiwa notes zake (au notes za mwalimu), na DIAR itajibu maswali yake sawa na notes hizo. Si majibu ya jumla kutoka mtandaoni, bali majibu yanayotegemea kile ambacho mwalimu alifundisha na kile mwanafunzi aliandika.
  • Walimu watatumia DIAR kutuma notes kwa wanafunzi. Badala ya kutuma faili au picha kupitia WhatsApp (ambayo mara nyingi hupotea, au inaleta kelele za group), mwalimu atapakia notes kwenye DIAR na wanafunzi watazipata kwa urahisi, kwa mpangilio, na wakiwa na uwezo wa kuuliza maswali juu yake.
  • Itasuluhisha mambo ya ofisi. Kutoka kupanga maelezo, kutoa feedback, hadi kufuatilia maendeleo ya wanafunzi – DIAR itasaidia kupunguza mzigo wa kiutawala.
  • Italeta mvuto wa elimu kwa wanachuo. Wanafunzi wataona teknolojia inayowahudumia moja kwa moja kulingana na mazingira yao, si AI ya kigeni inayotoa majibu ya nje.

Kwa ufupi, GPT ni AI iliyopo sasa yenye faida nyingi, lakini ina kasoro dhahiri katika tasisi za elimu – hasa kwa kuwa haitegemei yale yanayofundishwa darasani. DIAR, kama wazo, inalenga kujaza pengo hilo: kuwa mfumo unaofanya kazi ndani ya notes na mtaala wa chuo, na kuwawezesha walimu na wanafunzi kuwasiliana kwa njia bora zaidi.

Elimu Tanzania inahitaji teknolojia inayoelewa muktadha wetu. GPT imefungua mlango, lakini DIAR inaweza kuwa hatua inayofuata – ya ndani, ya notes, na ya kweli kwa wanafunzi na walimu wetu.

Comments